Thursday, February 17, 2011

MISAADA UWANJA WA UHURU KWA WAADHIRIKA WA MABOMU

 Mwamvita 3: Mkurugenzi wa mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akiwa amebeba  kapu lenye mikate kwa ajili ya waadhirika wa janga la ulipukaji wa mabomu Gongo la mboto waliopo katika kiwanja cha uhuru,Vodacom Foundation ilitoa misaada mbalimbali .
 Wafanyakazi Voda: Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wa Red Cross wakisaidiana kushusha vyakula mbalimbali katika lori lililosheheni  misaada  ya vyakula mbalimbali kwa ajili ya waadhirika wa janga la ulipukaji wa mabomu Gongo la mboto waliopo katika kiwanja cha uhuru.
Mtoto:Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiongea na mmoja wa watoto  waliopotezana na wazazi wao katika janga la ulipukaji wa mabomu Gongo la mboto, akiwa katika kiwanja cha uhuru mara baada ya wafanyakazi hao  kufika hapo kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More