Wednesday, February 23, 2011

Vodafone yachangia waathirika wa mabomu mil. 58/-



                                            
Vodafone Group Foundation imekabidhi hundi yenye thamani ya sh. milioni 58 kwa ajili ya waathirika wa milipuko ya mabomu iliyotokea wiki iliyopita katika kambi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Gongo la Mboto, Dar es Salaam.

Fedha hizo zimetolewa na Kitengo cha Maafa kinachosaidiwa na kuendeshwa na  Vodafone.

Mkuu wa kitengo hicho, Nick Red akizungumza na waliojeruhiwa na milipuko hiyo amesema tukio hilo ni baya kutokana na madhara yaliyotokea ikiwamo kupoteza maisha ya watu wengi.

"Inatia moyo kuona namna wafanyakazi wa Vodacom mlivyoitikia kuchangia wenzetu waliojeruhiwa katika tukio hili baya, tunaaini michango hii iliyotolewa na Vodafone Group pamoja na programu ya Red Alet misaada hii itaenda kusaidia kurejesha maisha ya wale waliojeruhiwa katika tukio hili," alisema.

Red alimkabidhi fedha hizo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki jana.
Read ni Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia Masoko Afrika, Mashariki ya Kati na Asia Pacific.

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare alisema kampuni yake itaendelea kusaidia waathirika wa milipuko hiyo ya mabomu Gongo la Mboto.

"Tumekuwa tukitoa misaada katika majanga mbalimbali yanayotokea nchini kupitia kitengo cha misaada na tutaendelea kufanya hivyo, pia umma unaombwa kuwasilisha michango yao kupitia kitengo hiki," alisema Mare.

Alisema kwa mtu yeyote anayetaka kuchangia kupitia kitengo hicho anatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye neno MAAFA na kutuma kwenda namba 15599.

Tukio la milipuko ya mabomu katika kambi ya JWTZ Gongo la Mboto, Dar es Salaam lilitokea usiku wa Jumatano ya Februari 16 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 25 na zaidi ya 400 kujeruhiwa.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More