Wednesday, March 2, 2011

VODACOM FOUNDATION BADO WAPO MONDULI!!

 Mkuu wa Wilaya ya Monduli  Bw.Jowika Kasunga  pamoja na Mkurugenzi  wa Mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba kulia wakifunua jiwe la msingi kuashiria makabidhiano rasmi ya jingo lenye madarasa mawili yaliyojengwa kwa msaada wa Vodacom Foundation katika shule ya Sekondary  ya wasichana ya  Irkisongo iliyopo wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kwa thamani ya shilingi Milioni 30.
 Mkurugenzi mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akipongezwa na wanafunzi wa shule ya Sekondary ya Irkisongo iliyopo wilaya ya Monduli Mkoani Arusha baada ya Mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom kukabidhi msaada wa Jengo lenye madarasa mawili yenye thamani ya shilingi  Milioni 30.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondary ya wasichana ya  Irkisongo iliyopo wilaya ya Monduli Mkoani Arusha,Happiness Nyange kulia akimwelezea jambo Mkurugenzi wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba mara baada ya kukabidhi msaada wa jengo lenye madarasa mawili yenye thamani ya shilingi Milioni 30,yaliyojengwa na Vodacom Foundation.

Mama Ika i can see mama Obama  ndani ya wewe.... ;)  keep it up maa

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More