Showing posts with label USHAURI. Show all posts
Showing posts with label USHAURI. Show all posts

Sunday, October 10, 2010

USHAURI TAFADHALI!!

Mie naomba ushauri, mimi ni mwanamke wa miaka 43 sasa ngozi yangu ina mafuta sana nafikiri ndio inaitwa sensitive skini sasa nilijaribu kutumia product zile za GNLD toka kipindi hicho ngozi yangu imekuwa na weusi kama nimeungua kuzunguka uso nimenitahidi nimeshindwa kila cream ninayoelekezwa kutumia nazidi ukwa mweusi na mie rangi yangu ni mweupe ingawa si mweupe sana yani nina ngozi ya kung'aa. Nisaidieni warembo nifanyeje jamani ili ngozi yangu irudi kama mwanzo?

MSHAURINI PLZ!!

Habari za kazi, mm ni mdada lakini nimeharibika sana shepu yangu kutokana na kuwa tumbo kubwa si kwamba niia mimba la hasha ni nyama nyingi na kadri siku zinavyokwenda linaongezeka taratibu naomba ushauri nifanyeje kukata tumbo? kwasababu inapelekea nashindwa hata kuvaa tops na nimeshajaribu kufanya  sit-ups, nimekunywa maji ya moto nimepunguza kula vyakula vya mafuta na beer lakini bado ngoma iko palepale

                                          NAOMBENI USHAURI WADAU

JE UNA TATIZO LA UREMBO AU MITINDO LINAKUTATIZO NA UNAHISI WADAU WAWEZA KUKUSHAURI TUMA VIA shamyomy@yahoo.com 

Thursday, October 7, 2010

USHAURI TAFADHALI!!

Kwanza naomba nikushukuru zeze kwa kutuwekea iyo picha ya dada anakwapa jeupe (Yenye kichwa cha habari , Mambo ya wax hayo), nilikuwa nawaza nitajielezaje nikawa nashindwa pa kuanzia.

Tafadhani mie nina tatizo hilo nina kwapa jeusi pamoja na najitahidi saana kunyoa japo sijawahi kujaribu kunyoa na wax nanyoa na shaving cream ya Nair ila ni jeusi tii.

nimeona wadau wametaja vitu vya kufanya (mfano hizo bleach, laser hair removal) naomba watuelekeze hapa(coz najua ni tatizo la wengi) watupe na majina yake na cost zake ili watu tupendeze  hata tukivaa nguo za wazi tuwe na comfidence za kunyanyua kwapa kupunga mkono.

Mama T

Monday, October 4, 2010

MSAIDIENI HUYU!!

shamy naomba msaada wako mm ni binti wa miaka 26 natarajia kufunga ndoa mwanzoni mwa mwaka ujao. sasa zeze nina tatizo la michirizi kwene mikono yangu na miguu japo miguu sio sana lakini hasa kwenye mikono nahofia kutovaa nguo ya wazi. sasa naomba unisaidie nipake nini ili michirizi iishe? mana  kuna filamu ya tafrani wema anaonekana kuharibika sana na hiyo michirizi lakini nimeangalia movie mpya ameekti na kanumba hivi majuzi kati hana hata alama hata moja ya michirizi sasa nashindwa kuwasiliana nae  mana sina contact zake anielekeze amepaka nini. plz naomba unisaidie dada yangu yani nakosa raha ya kuvaa nguo ya mikono mifupi.
wako mpenda blog yako
Nina

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More